expr:class='"loading" + data:blog.mobileClass'>
GABRIEL KILAMLYA NI BLOG AMBAYO INAKUPA WEWE NAFASI YA KUJUA MATUKIO YALIYOJILI MKOA WA NJOMBE NA DUNIANI KOTE KWA MAONI ZAIDI WASILIANA NASI KUPITIA gabrielkilamlya@gmail.com. KARIBUblog

Monday, July 22, 2013

 Wachekeshaji Maarufu Nchini TANZANIA Senga na Pembe wafanya kufuru Njombe.
 Msanii Maarufu wa Nyimbo za Injili Tanzania anayetamba na Wimbo wa Chaguo lako Vanessah Sanga akifanya Maonesho kwa wakazi wa Njombe
 Maelfu ya Wakazi wa Njombe wakimbilia Uwanjani Sabasaba Kushuhudia Mbwembwe za
Senga na Pembe.


 Wakazi wa Njombe wakiwa Kuangalia Tamasha la Injili hasa wachekeshaji Maarufu Nchini SENGA na Pembe.
Waimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania Kulia ni Vanessah Sanga Maarufu kwa Ngoma ya Chaguo lako akiwa na Enock Jonas Anayetamba na Wimbo wa Zunguka zunguka wakifanya yao katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Njombe Julai 21 Mwaka Huu.

Picha na Prosper Mfugale 

Tamasha la Injili Lililo andaliwa na MLOKOZI Intertainment Kutoka Mkoani Iringa Katika Uwanja wa Sabasaba Julai 21 Mwaka huu Limevunja Rekodi ya Kukonga Nyoyo za Mashabiki Hususani Pale walipo anza Mbwe mbwe akina SENGA NA PEMBE kATIKA Uwanja Huo Mjini Njombe.

Vichekesho vya Wachekeshaji Maarufu Kutoka Jijini Dar es Salaam WAKINA Pembe na Senga viliwaacha mashabiki Hoi wakiwa Stejini Katika Uwanja huo.

Pamoja na Tamasha Hilo Kuwaalika waimbaji wa Nyimbo za Injili Akiwemo Vanessah Sanga anayetamba na Wimbo wa Huyo ni chaguo Lako na Enock Jonas Anayetamba na Wimbo wa Zunguka zunguka ambao walialikwa Rasmi kwa ajili ya Tamasha Hilo Lakini Wachekeshaji hao walifanya kazi kubwa ya ziada ya Kujaza Mashabiki kwa Kiingilio cha Shilingi Elfu tatu kwa Elfu Mbili.

No comments:

Post a Comment